Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Sulaymān, amani imshukiye, akasema kumwambia mjumbe wa watu wa Saba’, «Rejea kwao, kwani naapa kwa Mwenyezi Mungu, tutawajia wao na askari wasioweza kupambana nao na kukabiliana nao, na tutawatoa kutoka nchini mwao wakiwa wadhalilifu, hali ya kuwa wanyonge wenye kudharauliwa, iwapo hawatafuata Dini ya Mwenyezi Mungu Peke Yake na hawataacha kumuabudu asiyekuwa Yeye.»