Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Alipokuja malkia wa Saba ’.kwa Sulaymān kwenye kikao chake aliambiwa, «je, kitanda cha ufalme wako kiko hivi?» Akasema, «Hicho kinafanana nacho.» Ikambainikia Sulaymān kuwa amejibu jawabu la sawa na ameshajua uweza wa Mwenyezi Mungu na usahihi wa unabii wa Sulaymān , amani imshukiye. Na tulipewa elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu na kujuwa uweza Wake kabla yake yeye, na tulikuwa ni wenye kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu ni wenye kuifuata dini ya Uislamu.»