. Na kwa kina Thamud tulimtuma ndugu yao Swaleh kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayo gombana. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika tulimtumiliza kwa watu wa Thamūd ndugu yao Ṣāliḥ kwamba: Mpwekesheni Mwenyezi Mungu na musimchukue mungu mwingine mukamuabudu pamoja na Yeye. Alipowajia Ṣāliḥ kuwalingania kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuabudu Peke Yake, watu wake walikuwa mapote mawili: mojawapo ya mapote mawili lilimuamini na lingine liliukanusha ulinganizi wake, kila mmoja kati ya watu wa mapote hayo mawili alikuwa akidai kwamba haki iko pamoja na yeye.