Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Naml 27:59

27:59
قل الحمد لله وسلام على عباده الذين اصطفى الله خير اما يشركون ٥٩
قُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلَـٰمٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ ٱلَّذِينَ ٱصْطَفَىٰٓ ۗ ءَآللَّهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ ٥٩
قُلِ
ٱلۡحَمۡدُ
لِلَّهِ
وَسَلَٰمٌ
عَلَىٰ
عِبَادِهِ
ٱلَّذِينَ
ٱصۡطَفَىٰٓۗ
ءَآللَّهُ
خَيۡرٌ
أَمَّا
يُشۡرِكُونَ
٥٩
Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha naye? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, «Sifa njema na shukrani ni za Mewenyezi Mungu, na amani kutoka Kwake na usalama ziwashukie waja Wake Aliowateua kwa kuwapa utume.» Kisha waulize washirikina wa watu wako, «Je, Mwenyezi Mungu Anayemiliki kunufaisha na kudhuru ni bora au ni yule wanayemshirikisha badala Yake kati ya wale wasiojimilikia wenyewe wala kuwamilikia wengine nafuu yoyote wala madhara yoyote?»