Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Naml 27:61

27:61
امن جعل الارض قرارا وجعل خلالها انهارا وجعل لها رواسي وجعل بين البحرين حاجزا االاه مع الله بل اكثرهم لا يعلمون ٦١
أَمَّن جَعَلَ ٱلْأَرْضَ قَرَارًۭا وَجَعَلَ خِلَـٰلَهَآ أَنْهَـٰرًۭا وَجَعَلَ لَهَا رَوَٰسِىَ وَجَعَلَ بَيْنَ ٱلْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا ۗ أَءِلَـٰهٌۭ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٦١
أَمَّن
جَعَلَ
ٱلۡأَرۡضَ
قَرَارٗا
وَجَعَلَ
خِلَٰلَهَآ
أَنۡهَٰرٗا
وَجَعَلَ
لَهَا
رَوَٰسِيَ
وَجَعَلَ
بَيۡنَ
ٱلۡبَحۡرَيۡنِ
حَاجِزًاۗ
أَءِلَٰهٞ
مَّعَ
ٱللَّهِۚ
بَلۡ
أَكۡثَرُهُمۡ
لَا
يَعۡلَمُونَ
٦١
Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, kuviabudu vile mnavyovishirikisha na Mola wenu ni bora au Yule Aliyewafanyia ardhi kuwa ni mahali pa kutulia, Akaitoa mito kati yake, Akaiwekea majabali yaliyojikita na Akaweka kizuizi baina ya bahari mbili, ya tamu na chumvi, ili mojawapo isiiharibu nyingine? Je kuna muabudiwa yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu alifanya hilo hata mumshirikishe na Yeye katika kuabudu kwenu? Bali wengi wa hawa washirikina hawajui kadiri ya ukubwa wa Mwenyezi Mungu, hivyo basi wanamshirikisha Yeye kwa kuiga na kwa udhalimu.