Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Naml 27:64

27:64
امن يبدا الخلق ثم يعيده ومن يرزقكم من السماء والارض االاه مع الله قل هاتوا برهانكم ان كنتم صادقين ٦٤
أَمَّن يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۗ أَءِلَـٰهٌۭ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ ٦٤
أَمَّن
يَبۡدَؤُاْ
ٱلۡخَلۡقَ
ثُمَّ
يُعِيدُهُۥ
وَمَن
يَرۡزُقُكُم
مِّنَ
ٱلسَّمَآءِ
وَٱلۡأَرۡضِۗ
أَءِلَٰهٞ
مَّعَ
ٱللَّهِۚ
قُلۡ
هَاتُواْ
بُرۡهَٰنَكُمۡ
إِن
كُنتُمۡ
صَٰدِقِينَ
٦٤
Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na waulize wao: Ni nani anayeanzisha kuumba viumbe, kisha anaviondosha akitaka, kisha anavirudisha? Na ni nani anayewaruzuku nyinyi kutoka mbinguni kwa kuiteremsha mvua? Na ni nani anayehuisha ardhi kwa kuotesha mimea na vinginevyo? Je, kuna muabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu anafanya hayo? Sema, Leteni hoja yenu iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu kwamba Mwenyezi Mungu Ana mshirika katika mamlaka Yake na ibada Yake.»