Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Naml 27:80

27:80
انك لا تسمع الموتى ولا تسمع الصم الدعاء اذا ولوا مدبرين ٨٠
إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ ٱلْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا وَلَّوْا۟ مُدْبِرِينَ ٨٠
إِنَّكَ
لَا
تُسۡمِعُ
ٱلۡمَوۡتَىٰ
وَلَا
تُسۡمِعُ
ٱلصُّمَّ
ٱلدُّعَآءَ
إِذَا
وَلَّوۡاْ
مُدۡبِرِينَ
٨٠
Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie, wala kuwafanya viziwi wasikie wito, wanapo kwisha geuka kwenda zao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika yako wewe, ewe Mtume, huwezi kumsikilizisha haki yule ambaye Mwenyezi Mungu Amepiga mhuri juu ya moyo wake Akaufisha, na humsikilizishi ulinganizi wako yule ambaye Mwenyezi Mungu Ameyafanya masikizi yake kuwa kiziwi asiisikie haki, pindi wanapogeuka kukupa mgongo wewe. Kwani kiziwi hasikii ulinganizi akiwa amekuelekea, basi itakuwa vipi akiwa katika hali ya kupa mgongo na kugeuka?