Wala huwezi kuwaongoa vipofu waache upotovu wao. Huwezi kuwafanya wasikie isipo kuwa wenye kuziamini Ishara zetu; na hao ndio wat'iifu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wewe, ewe Mtume, hukuwa ni mwenye kuongoa kutoka kwenye upotevu yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemfanya kipofu asiuone uongofu na unyofu. Na haimkini kwako wewe umsikilizishe isipokuwa yule anayeziamini aya zetu, basi hao ni wenye kusalimu amri, watiifu na wenye kuyakubali yale ninayowalingania wao.