Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa makhaaini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sisi tumekuteremshia Qur’ani, ewe Muhammad, iliyokusanya haki, ili utoe uamuzi baina ya watu wote kwa wahyi ambao Mwenyezi Mungu Amekuletea na Akakufahamisha. Basi usiwe ni mwenye kuwatetea wale wanaozifanyia hiana nafsi zao, kwa kuificha haki, kwa kuwa wamekudhihirishia maneno yaliyo kinyume na ukweli.