Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:108

4:108
يستخفون من الناس ولا يستخفون من الله وهو معهم اذ يبيتون ما لا يرضى من القول وكان الله بما يعملون محيطا ١٠٨
يَسْتَخْفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ ٱلْقَوْلِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ١٠٨
يَسۡتَخۡفُونَ
مِنَ
ٱلنَّاسِ
وَلَا
يَسۡتَخۡفُونَ
مِنَ
ٱللَّهِ
وَهُوَ
مَعَهُمۡ
إِذۡ
يُبَيِّتُونَ
مَا
لَا
يَرۡضَىٰ
مِنَ
ٱلۡقَوۡلِۚ
وَكَانَ
ٱللَّهُ
بِمَا
يَعۡمَلُونَ
مُحِيطًا
١٠٨
Wanataka kujificha kwa watu, wala hawataki kujificha kwa Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapo panga njama usiku kwa maneno asiyo yapenda. Na Mwenyezi Mungu anayajua vyema wanayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wao wanajificha na watu ili wasipate kuyaona matendo yao mabaya, wala hawajifichi na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka wala hawamuonei haya, ilhali Yeye, Mtukufu wa mambo, Yupo na wao kwa ujuzi Wake, Anawaona wanapopanga, kipindi cha usiku, maneno Asiyoridhika nayo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameyazunguka(kwa ujuzi Kwake) maneno yao yote na vitendo vyao vyote, hakuna kitu chochote chenye kufichika Kwake.