Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:119

4:119
ولاضلنهم ولامنينهم ولامرنهم فليبتكن اذان الانعام ولامرنهم فليغيرن خلق الله ومن يتخذ الشيطان وليا من دون الله فقد خسر خسرانا مبينا ١١٩
وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَـَٔامُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ ءَاذَانَ ٱلْأَنْعَـٰمِ وَلَـَٔامُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيْطَـٰنَ وَلِيًّۭا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًۭا مُّبِينًۭا ١١٩
وَلَأُضِلَّنَّهُمۡ
وَلَأُمَنِّيَنَّهُمۡ
وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ
فَلَيُبَتِّكُنَّ
ءَاذَانَ
ٱلۡأَنۡعَٰمِ
وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ
فَلَيُغَيِّرُنَّ
خَلۡقَ
ٱللَّهِۚ
وَمَن
يَتَّخِذِ
ٱلشَّيۡطَٰنَ
وَلِيّٗا
مِّن
دُونِ
ٱللَّهِ
فَقَدۡ
خَسِرَ
خُسۡرَانٗا
مُّبِينٗا
١١٩
Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Na nitawaepusha na haki wenye kunifuata, nitawaahidi kwa urongo mambo wanayoyatamani, nitawaita wayakate na kuyapasua masikio ya wanyama-hoa kwa kuwapambia walifanye jambo hili la ubatili na nitawalingania wageuze umbo la Mwenyezi Mungu Alilowaumbia nalo katika tabia za kimaumbile na hali ya viumbe vile walivyo.» Na mwenye kukubali mwito wa Shetani na kumfanya yeye ndiye muokozi wake badala ya Mwenyezi Mungu, ameangamia maangamivu yaliyo wazi.