Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipo kuwa Mwenyezi Mungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Fadhila hizi kubwa hazipatikani kwa matamanio mnayoyatamani, enyi Waislamu, wala kwa matamanio ya Mayahudi na Wanaswara waliopewa Kitabu. Hakika zinapatikana kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kikweli na kuyafanya vizuri matendo ya kumridhisha. Na yoyote mwenye kufanya tendo baya, atalipwa kwalo, na hatompata, asiyekuwa Mwenyezi Mungu, mtegemewa mwenye kusimamia mambo yake wala msaidizi mwenye kumnusuru na kumuepushia adhabu mbaya.