Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:129

4:129
ولن تستطيعوا ان تعدلوا بين النساء ولو حرصتم فلا تميلوا كل الميل فتذروها كالمعلقة وان تصلحوا وتتقوا فان الله كان غفورا رحيما ١٢٩
وَلَن تَسْتَطِيعُوٓا۟ أَن تَعْدِلُوا۟ بَيْنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا۟ كُلَّ ٱلْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورًۭا رَّحِيمًۭا ١٢٩
وَلَن
تَسۡتَطِيعُوٓاْ
أَن
تَعۡدِلُواْ
بَيۡنَ
ٱلنِّسَآءِ
وَلَوۡ
حَرَصۡتُمۡۖ
فَلَا
تَمِيلُواْ
كُلَّ
ٱلۡمَيۡلِ
فَتَذَرُوهَا
كَٱلۡمُعَلَّقَةِۚ
وَإِن
تُصۡلِحُواْ
وَتَتَّقُواْ
فَإِنَّ
ٱللَّهَ
كَانَ
غَفُورٗا
رَّحِيمٗا
١٢٩
Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hamtaweza, enyi wanaume, kuhakikisha uadilifu kamili wa mapenzi na muelekeo wa moyo kati ya wanawake, namna mtakavyofanya bidii juu ya hilo. Basi msimpe mgongo, yule msiokuwa na haja naye, kabisa-kabisa mkamuacha akawa ni kama mwanamke ambaye hana mume wala hakutalikiwa, mkaja mkapata madhambi. Na mkizitengeneza amali zenu mkafanya uadilifu katika ugawaji wenu baina ya wake zenu na mkamchunga Mwenyezi Mungu mkamuogopa juu yao, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao.