Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:131

4:131
ولله ما في السماوات وما في الارض ولقد وصينا الذين اوتوا الكتاب من قبلكم واياكم ان اتقوا الله وان تكفروا فان لله ما في السماوات وما في الارض وكان الله غنيا حميدا ١٣١
وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا۟ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَنِيًّا حَمِيدًۭا ١٣١
وَلِلَّهِ
مَا
فِي
ٱلسَّمَٰوَٰتِ
وَمَا
فِي
ٱلۡأَرۡضِۗ
وَلَقَدۡ
وَصَّيۡنَا
ٱلَّذِينَ
أُوتُواْ
ٱلۡكِتَٰبَ
مِن
قَبۡلِكُمۡ
وَإِيَّاكُمۡ
أَنِ
ٱتَّقُواْ
ٱللَّهَۚ
وَإِن
تَكۡفُرُواْ
فَإِنَّ
لِلَّهِ
مَا
فِي
ٱلسَّمَٰوَٰتِ
وَمَا
فِي
ٱلۡأَرۡضِۚ
وَكَانَ
ٱللَّهُ
غَنِيًّا
حَمِيدٗا
١٣١
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ni milki ya Mwenyezi Mungu vilivyoko kwenye mbingu na vilivyoko kwenye ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili. Na tuliwausia wale waliopewa Vitabu kabla yenu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, na tukawausia nyinyi pia, enyi ummah wa Muhammad, mumche Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na msimame kutekeleza amri Zake na kuepuka makatazo Yake, na tukawaelezea kwamba nyinyi mkiukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na sheria Zake, basi Mwenyezi Mungu Hawahitajii nyinyi, kwa kuwa vyote vilivyoko kwenye mbingu na vilivyoko kwenye ardhi ni Vyake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha kutowahitjia viumbe Wake, ni Mwingi wa kuhimidiwa katika sifa Zake na vitendo Vyake.