Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:140

4:140
وقد نزل عليكم في الكتاب ان اذا سمعتم ايات الله يكفر بها ويستهزا بها فلا تقعدوا معهم حتى يخوضوا في حديث غيره انكم اذا مثلهم ان الله جامع المنافقين والكافرين في جهنم جميعا ١٤٠
وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِى ٱلْكِتَـٰبِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا۟ مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا۟ فِى حَدِيثٍ غَيْرِهِۦٓ ۚ إِنَّكُمْ إِذًۭا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ جَامِعُ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱلْكَـٰفِرِينَ فِى جَهَنَّمَ جَمِيعًا ١٤٠
وَقَدۡ
نَزَّلَ
عَلَيۡكُمۡ
فِي
ٱلۡكِتَٰبِ
أَنۡ
إِذَا
سَمِعۡتُمۡ
ءَايَٰتِ
ٱللَّهِ
يُكۡفَرُ
بِهَا
وَيُسۡتَهۡزَأُ
بِهَا
فَلَا
تَقۡعُدُواْ
مَعَهُمۡ
حَتَّىٰ
يَخُوضُواْ
فِي
حَدِيثٍ
غَيۡرِهِۦٓ
إِنَّكُمۡ
إِذٗا
مِّثۡلُهُمۡۗ
إِنَّ
ٱللَّهَ
جَامِعُ
ٱلۡمُنَٰفِقِينَ
وَٱلۡكَٰفِرِينَ
فِي
جَهَنَّمَ
جَمِيعًا
١٤٠
Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnapo sikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanaafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannamu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mola wenu Amewateremshia, enyi Waumini, katika Kitabu Chake kwamba mkisikia aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na zinafanyiwa shere, basi msikae pamoja na wakanushaji hao wanaofanya shere, isipokuwa wakiingia kwenye mazungumzo yasiokuwa mazungumzo ya kukanusha na kuzifanyia shere aya za Mwenyezi Mungu. Nyinyi mkikaa nao, na wao wako katika hali hiyo, mtakuwa ni kama wao, kwa kuwa nyinyi mmeridhika na ukafiri wao na uchezaji shere wao. Na mwenye kuridhika na maasia ni kama mwenye kuyafanya. Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mwenye Atawakusanya wanafiki na makafiri wote ndani ya Moto wa Jahanamu ambapo humo watakumbana na ukali wa adhabu.