Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:142

4:142
ان المنافقين يخادعون الله وهو خادعهم واذا قاموا الى الصلاة قاموا كسالى يراءون الناس ولا يذكرون الله الا قليلا ١٤٢
إِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ يُخَـٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَـٰدِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوٓا۟ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُوا۟ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلًۭا ١٤٢
إِنَّ
ٱلۡمُنَٰفِقِينَ
يُخَٰدِعُونَ
ٱللَّهَ
وَهُوَ
خَٰدِعُهُمۡ
وَإِذَا
قَامُوٓاْ
إِلَى
ٱلصَّلَوٰةِ
قَامُواْ
كُسَالَىٰ
يُرَآءُونَ
ٱلنَّاسَ
وَلَا
يَذۡكُرُونَ
ٱللَّهَ
إِلَّا
قَلِيلٗا
١٤٢
Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kuswali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika mbinu ya wanafiki hawa ni kumhadaa Mwenyezi Mungu kwa Imani wanaojionyesha nayo na ukafiri wanaouficha, kwa kudhani kuwa mbinu yao itafichamana kwa Mwenyezi Mungu, na hali ni kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Anayewahadaa na ni Mwenye kuwalipa malipo yanayofanana na vitendo vyao. Wanafiki hawa wanaposimama kutekeleza Swala, wanasimama kufanya hivyo kwa uvivu, wanakusudia, kwa kuswali kwao, kuonekena na kusikika. Na wao hawamtaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, isipokuwa kumtaja kwa uchache.