MWENYEZI MUNGU hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hapendi Mwenyezi Mungu kwa yoyote adhihirishe neno ovu. Lakini yaruhusiwa kwa aliyedhulumiwa amtaje aliyemdhulumu kwa uovu alionao, ili akibainishe alichodhulumiwa nacho. Na daima Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia mnayoyadhihirisha na ni Mwenye kuyajua mnayoyaficha kati ya hayo.