Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:149

4:149
ان تبدوا خيرا او تخفوه او تعفوا عن سوء فان الله كان عفوا قديرا ١٤٩
إِن تُبْدُوا۟ خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا۟ عَن سُوٓءٍۢ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّۭا قَدِيرًا ١٤٩
إِن
تُبۡدُواْ
خَيۡرًا
أَوۡ
تُخۡفُوهُ
أَوۡ
تَعۡفُواْ
عَن
سُوٓءٖ
فَإِنَّ
ٱللَّهَ
كَانَ
عَفُوّٗا
قَدِيرًا
١٤٩
Mkidhihirisha wema au mkiuficha, au mkiyasamehe maovu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Muweza. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Amehimiza Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwamba watu wasamehe, na Akaweka msingi wa jambo hilo kwa kuwa Muumini, ima aidhihirishe kheri au aifiche. Na vilevile katika kukosewa, ima adhihirishe kuwa amekosewa katika hali ya kutafuta haki yake kwa aliyemkosea au asamehe na apuuze. Na kusamehe ni bora. Kwani miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu ni kuwasamehe waja Wake pamoja na uwezo Wake juu yao.