Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:153

4:153
يسالك اهل الكتاب ان تنزل عليهم كتابا من السماء فقد سالوا موسى اكبر من ذالك فقالوا ارنا الله جهرة فاخذتهم الصاعقة بظلمهم ثم اتخذوا العجل من بعد ما جاءتهم البينات فعفونا عن ذالك واتينا موسى سلطانا مبينا ١٥٣
يَسْـَٔلُكَ أَهْلُ ٱلْكِتَـٰبِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَـٰبًۭا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا۟ مُوسَىٰٓ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوٓا۟ أَرِنَا ٱللَّهَ جَهْرَةًۭ فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ ٱتَّخَذُوا۟ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَءَاتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَـٰنًۭا مُّبِينًۭا ١٥٣
يَسۡـَٔلُكَ
أَهۡلُ
ٱلۡكِتَٰبِ
أَن
تُنَزِّلَ
عَلَيۡهِمۡ
كِتَٰبٗا
مِّنَ
ٱلسَّمَآءِۚ
فَقَدۡ
سَأَلُواْ
مُوسَىٰٓ
أَكۡبَرَ
مِن
ذَٰلِكَ
فَقَالُوٓاْ
أَرِنَا
ٱللَّهَ
جَهۡرَةٗ
فَأَخَذَتۡهُمُ
ٱلصَّٰعِقَةُ
بِظُلۡمِهِمۡۚ
ثُمَّ
ٱتَّخَذُواْ
ٱلۡعِجۡلَ
مِنۢ
بَعۡدِ
مَا
جَآءَتۡهُمُ
ٱلۡبَيِّنَٰتُ
فَعَفَوۡنَا
عَن
ذَٰلِكَۚ
وَءَاتَيۡنَا
مُوسَىٰ
سُلۡطَٰنٗا
مُّبِينٗا
١٥٣
Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wanakutaka Mayahudi, ewe Mtume, uwaonyeshe miujiza mfano wa miujiza ya Mūsā iwe ni ushahidi kwako kuwa ni mkweli, nao ni uwateremshie kurasa zitokazo kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa zimeandikwa, kama vile Mūsā alivyoleta mbao kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Usione ajabu, ewe Mtume, kwani wakale wao walimtaka Mūsā, amani imshukie, awaletee makubwa zaidi. Walimtaka Awaonyeshe Mwenyezi Mungu waziwazi, hapo wakateremshiwa moto uliowaua kwa sababu ya kuzidhulumu nafsi zao walipolitaka jambo ambalo si haki yao. Na baada ya Mwenyezi Mungu kuwahuisha, baada ya kufa kwao, na wakaishuhudia miujiza iliyo waziwazi, kutoka kwa Mtume Mūsā, inayopinga katakata ushirikina, waliabuduu kigombe badala ya Mwenyezi Mungu. Kisha tuliwasamehe kosa lao la kuabudu ndama kwa sababu ya kutubia kwao na tukampa Mūsā hoja kubwa zilizotilia nguvu ukweli wa utume wake