Na kuchukua kwao riba, nao wamekatazwa, na kula kwao mali ya watu kwa dhulma. Basi tumewaandalia makafiri katika wao adhabu yenye uchungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kwa sababu ya kutumia kwao riba ambayo walikatazwa wasitumie na kujihalalishia kwao mali za watu pasi na haki. Na tumewatayarishia waliomkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake adhabu iumizayo huko Akhera.