Lakini Mwenyezi Mungu anayashuhudia aliyo kuteremshia wewe. Ameyateremsha kwa kujua kwake - na Malaika pia wanashuhudia. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Iwapo Mayahudi na wengineo watakukanusha, ewe Mtume, hakika Mwenyezi Mungu Anashuhudia kuwa wewe ni Mtume Wake Aliyemteremshia Qur’ani tukufu; Ameiteremsha kwa ujuzi Wake. Na vilevile Malaika wanashuhudia ukweli wa wahyi uliyoletewa. Na ushahidi wa Mwenyezi Mungu Peke Yake unatosha.