Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:22

4:22
ولا تنكحوا ما نكح اباوكم من النساء الا ما قد سلف انه كان فاحشة ومقتا وساء سبيلا ٢٢
وَلَا تَنكِحُوا۟ مَا نَكَحَ ءَابَآؤُكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ فَـٰحِشَةًۭ وَمَقْتًۭا وَسَآءَ سَبِيلًا ٢٢
وَلَا
تَنكِحُواْ
مَا
نَكَحَ
ءَابَآؤُكُم
مِّنَ
ٱلنِّسَآءِ
إِلَّا
مَا
قَدۡ
سَلَفَۚ
إِنَّهُۥ
كَانَ
فَٰحِشَةٗ
وَمَقۡتٗا
وَسَآءَ
سَبِيلًا
٢٢
Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wala msiwaoe wanawake walioolewa na baba zenu, isipokuwa yaliyopita mliyoyafanya katika zama za jahiliyyah (kabla ya Uislamu). Hayo hamtalipwa kwayo. Hakika ndoa ya watoto kuwaoa waliokuwa wake wa baba zao ni jambo baya lenye upeo wa ubaya, na ni jambo lenye kuchukiza ambalo Mwenyezi Mungu Anamchukia mwenye kulifanya. Na ubaya wa njia na mwenendo ni huo mliokuwa mkiufanya zama za ujinga wenu( kabla ya Uislamu).