Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mkijiepusha, enyi Waumini, na madhambi makubwa, kama kumshrikisha Mwenyezi Mungu, kuwaasi wazazi wawili, kumuua mtu bila ya haki na mengineyo, tutawasamehe madhambi yenu madogo yaliyo chini ya hayo na tutawaingiza mahali pema pa kuingia, napo ni Pepo.