Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:33

4:33
ولكل جعلنا موالي مما ترك الوالدان والاقربون والذين عقدت ايمانكم فاتوهم نصيبهم ان الله كان على كل شيء شهيدا ٣٣
وَلِكُلٍّۢ جَعَلْنَا مَوَٰلِىَ مِمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ ۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ فَـَٔاتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍۢ شَهِيدًا ٣٣
وَلِكُلّٖ
جَعَلۡنَا
مَوَٰلِيَ
مِمَّا
تَرَكَ
ٱلۡوَٰلِدَانِ
وَٱلۡأَقۡرَبُونَۚ
وَٱلَّذِينَ
عَقَدَتۡ
أَيۡمَٰنُكُمۡ
فَـَٔاتُوهُمۡ
نَصِيبَهُمۡۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
كَانَ
عَلَىٰ
كُلِّ
شَيۡءٖ
شَهِيدًا
٣٣
Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea warithi wenye kukirithi kilichoachwa na wazazi wawili na jamaa wa karibu. Na wale mliofungamana nao kwa mayamini yaliyotiliwa mkazo kuwa mtanusuriana na mtawapa kitu katika urithi, basi wapeni walichokadiriwa. Kurithiana kwa mikataba ya kunusuriana kulikuwako mwanzo wa Uislamu , kisha hukumu yake ikaondolewa kwa kuteremka aya za mirathi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila kitu katika vitendo vyenu na Atawalipa kulingana navyo.