Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:35

4:35
وان خفتم شقاق بينهما فابعثوا حكما من اهله وحكما من اهلها ان يريدا اصلاحا يوفق الله بينهما ان الله كان عليما خبيرا ٣٥
وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَٱبْعَثُوا۟ حَكَمًۭا مِّنْ أَهْلِهِۦ وَحَكَمًۭا مِّنْ أَهْلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصْلَـٰحًۭا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيْنَهُمَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًۭا ٣٥
وَإِنۡ
خِفۡتُمۡ
شِقَاقَ
بَيۡنِهِمَا
فَٱبۡعَثُواْ
حَكَمٗا
مِّنۡ
أَهۡلِهِۦ
وَحَكَمٗا
مِّنۡ
أَهۡلِهَآ
إِن
يُرِيدَآ
إِصۡلَٰحٗا
يُوَفِّقِ
ٱللَّهُ
بَيۡنَهُمَآۗ
إِنَّ
ٱللَّهَ
كَانَ
عَلِيمًا
خَبِيرٗا
٣٥
Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mkijua, enyi wasimamizi wa mume na mke, kuwa kuna ugomvi baina yao unaopelekea kutengana, wapelekeeni mwamuzi muadilifu wa upande wa mume na mwamuzi muadilifu wa upande wa mke, ili watazame na kutoa uamuzi wenye maslahi ya wao wawili. Na kwa kuwa wale waamuzi wawili wana hamu ya kupatanisha na wanatumia njia nzuri, Mwenyezi Mungu Atawatilia taufiki baina ya mume na mke. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, hakuna chochote kinachofichamana Kwake kuhusu mambo ya waja Wake, ni Mtambuzi wa yaliyomo ndani ya nafsi zao.