Na ingeli wadhuru nini wao lau wangeli muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwani kuna madhara gani yatakayowafika wao lau walimuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, kiitikadi na kivitendo, na wakayatoa yale Aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa kutaka thawabu na kuwa na ikhlasi. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kuwajua wao na kuyajua wayafanyayo na Atawahesabu kwayo.