Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wapeni wanawake, enyi waume, mahari yao, kipewa kinacholazimu na faradhi iliyopasa, kwa roho yenu safi. Na iwapo zitakuwa safi nafsi zao kwenu na kuwatunuku chochote katika mahari, basi kichukueni na mkitumie mnavyotaka, kwani hicho ni halali iliyo nzuri.