Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:40

4:40
ان الله لا يظلم مثقال ذرة وان تك حسنة يضاعفها ويوت من لدنه اجرا عظيما ٤٠
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍۢ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةًۭ يُضَـٰعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًۭا ٤٠
إِنَّ
ٱللَّهَ
لَا
يَظۡلِمُ
مِثۡقَالَ
ذَرَّةٖۖ
وَإِن
تَكُ
حَسَنَةٗ
يُضَٰعِفۡهَا
وَيُؤۡتِ
مِن
لَّدُنۡهُ
أَجۡرًا
عَظِيمٗا
٤٠
Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja. Na ikiwa ni jambo jema basi Yeye hulizidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Hampunguzii yoyote malipo ya matendo yake hata kama ni kadiri ya chungu. Na uwapo huo uzito wa chungu ni jambo jema, basi Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa pungufu, Atamuongezea na kumkuzia mwenye kulifanya, na Atamkirimu kwa nyongeza, kwa kumpa kutoka Kwake thawabu kubwa ambazo ni Pepo.