Tazama vipi wanavyo mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na haya yatosha kuwa dhambi iliyo dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Watazame, ewe Mtume, kwa kuyaonea ajabu mambo yao, vipi wanamzulia Mwenyezi Mungu urongo, na hali Yeye Ndiye Anayetakaswa na kila lisilokuwa laiki na Yeye? Uzushi huu unatosha kuwa ni dhambi kubwa lenye kuonyesha wazi itikadi yao mbovu.