Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:57

4:57
والذين امنوا وعملوا الصالحات سندخلهم جنات تجري من تحتها الانهار خالدين فيها ابدا لهم فيها ازواج مطهرة وندخلهم ظلا ظليلا ٥٧
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّـٰتٍۢ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًۭا ۖ لَّهُمْ فِيهَآ أَزْوَٰجٌۭ مُّطَهَّرَةٌۭ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّۭا ظَلِيلًا ٥٧
وَٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
وَعَمِلُواْ
ٱلصَّٰلِحَٰتِ
سَنُدۡخِلُهُمۡ
جَنَّٰتٖ
تَجۡرِي
مِن
تَحۡتِهَا
ٱلۡأَنۡهَٰرُ
خَٰلِدِينَ
فِيهَآ
أَبَدٗاۖ
لَّهُمۡ
فِيهَآ
أَزۡوَٰجٞ
مُّطَهَّرَةٞۖ
وَنُدۡخِلُهُمۡ
ظِلّٗا
ظَلِيلًا
٥٧
Na wale walio amini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito kati yake kwa kudumu humo milele. Huko watakuwa na wake walio takasika, na tutawaingiza katika vivuli vizuri kweli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wale ambao nyoyo zao zilitulia kwa kumuamini Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kuukubali ujumbe wa Mtume Wake, Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na wakasimama imara juu ya utiifu, tutawaingiza kwenye mabustani ya Pepo ambayo, chini ya majumba yake ya fahari na miti yake, inapita mito. Watastarehe humo milele na hawatatoka humo. Watakuwa na wake humo waliotakaswa na Mwenyezi Mungu na kila maudhi. Na tutawatia kwenye vivuli vilivyoshikana vilivyorefuka Peponi.