Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:78

4:78
اينما تكونوا يدرككم الموت ولو كنتم في بروج مشيدة وان تصبهم حسنة يقولوا هاذه من عند الله وان تصبهم سيية يقولوا هاذه من عندك قل كل من عند الله فمال هاولاء القوم لا يكادون يفقهون حديثا ٧٨
أَيْنَمَا تَكُونُوا۟ يُدْرِككُّمُ ٱلْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِى بُرُوجٍۢ مُّشَيَّدَةٍۢ ۗ وَإِن تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌۭ يَقُولُوا۟ هَـٰذِهِۦ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌۭ يَقُولُوا۟ هَـٰذِهِۦ مِنْ عِندِكَ ۚ قُلْ كُلٌّۭ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ ۖ فَمَالِ هَـٰٓؤُلَآءِ ٱلْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًۭا ٧٨
أَيۡنَمَا
تَكُونُواْ
يُدۡرِككُّمُ
ٱلۡمَوۡتُ
وَلَوۡ
كُنتُمۡ
فِي
بُرُوجٖ
مُّشَيَّدَةٖۗ
وَإِن
تُصِبۡهُمۡ
حَسَنَةٞ
يَقُولُواْ
هَٰذِهِۦ
مِنۡ
عِندِ
ٱللَّهِۖ
وَإِن
تُصِبۡهُمۡ
سَيِّئَةٞ
يَقُولُواْ
هَٰذِهِۦ
مِنۡ
عِندِكَۚ
قُلۡ
كُلّٞ
مِّنۡ
عِندِ
ٱللَّهِۖ
فَمَالِ
هَٰٓؤُلَآءِ
ٱلۡقَوۡمِ
لَا
يَكَادُونَ
يَفۡقَهُونَ
حَدِيثٗا
٧٨
Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu. Na likiwafikilia jema wanasema: Hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na likiwafikilia ovu wanasema: Hili limetoka kwako wewe. Sema: Yote yanatokana na Mwenyezi Mungu. Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Popote mliopo mtafikiwa na kifo, pawe ni mahali popote pale mnapokuwa, muda wenu ukikoma, hata kama mupo ndani ya ngome zilizoimarishwa zilizoko mbali na kiwanja cha mapambano na mapigano. Na wakipatikana na mambo ya kuwafurahisha ya starehe ya maisha haya (ya ulimwenguni), wanayanasibisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kuwa Ndiye Aliyewapatia, na watokewapo na matukio wanayoyachukia, wanayanasibisha kwa Mtume Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwa yamesababishwa na yeye kwa ujinga wao na kwa fikira zao kuwa yeye amewaletea nuhusi. Na hawakujua kwamba yote yanatokana na Mwenyezi Mungu Peke Yake, kwa uamuzi Wake na makadirio Yake. Basi kwa nini wao hawakaribii kuelewa maneno yoyote unayowaelezea?