Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:79

4:79
ما اصابك من حسنة فمن الله وما اصابك من سيية فمن نفسك وارسلناك للناس رسولا وكفى بالله شهيدا ٧٩
مَّآ أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍۢ فَمِنَ ٱللَّهِ ۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍۢ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَـٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولًۭا ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۭا ٧٩
مَّآ
أَصَابَكَ
مِنۡ
حَسَنَةٖ
فَمِنَ
ٱللَّهِۖ
وَمَآ
أَصَابَكَ
مِن
سَيِّئَةٖ
فَمِن
نَّفۡسِكَۚ
وَأَرۡسَلۡنَٰكَ
لِلنَّاسِ
رَسُولٗاۚ
وَكَفَىٰ
بِٱللَّهِ
شَهِيدٗا
٧٩
Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Chochote kinachokupata, ewe binadamu, cha wema na neema, kinatoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Peke Yake, kwa ukarimu na hisani. Na chochote kinachokufika cha tabu na mashaka ni kwa sababu ya vitendo vyako vibaya na makosa na madhambi yaliyotendwa na mikono yako miwili. Na tumekutumiliza, ewe Mtume, kuwa ni Mtume kwa watu wote uwafikishie ujumbe wa Mola wako. Na inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya ukweli wa utume Wako.