Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yoyote mwenye kumkubali Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na akafuata uongofu wake kivitendo, basi amemkubali Mwenyezi mungu Aliyetukuka na amefuata amri Yake. Na yoyote aliyekataa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi hatukukutumiliza, ewe Mtume, kwa hawa wenye kukataa uwe ni mtunzi wa kuyadhibiti matendo yao na kuwahesabu kwa hayo. Hesabu yao ni juu yetu.