Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:81

4:81
ويقولون طاعة فاذا برزوا من عندك بيت طايفة منهم غير الذي تقول والله يكتب ما يبيتون فاعرض عنهم وتوكل على الله وكفى بالله وكيلا ٨١
وَيَقُولُونَ طَاعَةٌۭ فَإِذَا بَرَزُوا۟ مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَآئِفَةٌۭ مِّنْهُمْ غَيْرَ ٱلَّذِى تَقُولُ ۖ وَٱللَّهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا ٨١
وَيَقُولُونَ
طَاعَةٞ
فَإِذَا
بَرَزُواْ
مِنۡ
عِندِكَ
بَيَّتَ
طَآئِفَةٞ
مِّنۡهُمۡ
غَيۡرَ
ٱلَّذِي
تَقُولُۖ
وَٱللَّهُ
يَكۡتُبُ
مَا
يُبَيِّتُونَۖ
فَأَعۡرِضۡ
عَنۡهُمۡ
وَتَوَكَّلۡ
عَلَى
ٱللَّهِۚ
وَكَفَىٰ
بِٱللَّهِ
وَكِيلًا
٨١
Na wanasema: Tunat'ii. Lakini wanapo toka kwako kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayo yasema. Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayo yapangia njama za usiku. Basi waachilie mbali, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hawa wenye kukataa, wakiwa kwenye baraza ya Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wanajidhihirisha kuwa wanamtii Mtume na kuyafuata yale aliyokuja nayo, na wakiwa mbali na yeye na wakaondoka kwenye baraza yake, linatoka kundi katika wao likapanga njama kinyume cha yale waliyoyadhihirisha ya kumtii. Na wao hawakujua kwamba Mwenyezi Mungu Anadhibiti hesabu ya yale wanayoyapanga na kwamba Yeye Atawalipa kwa hayo malipo kamili. Basi wape mgongo na usiwajali, kwani wao hawatakudhuru. Na tegemea kwa Mwenyezi Mungu, kwani yeye Peke Yake Ndiye Mwenye kukutosha kwa usimamizi na utetezi.