Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwani hawa hawaiangalii Qur’ani na haki iliyokuja nayo, kwa kuitaamali na kuizingatia, namna ilivyokuja kwa utaratibu uliopangika unaomfanya mtu awe na yakini kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake? Na lau yalikuwa yatoka kwa asiyekuwa Yeye, wangalipata ndani yake tafauti kubwa.