Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nisaa 4:96

4:96
درجات منه ومغفرة ورحمة وكان الله غفورا رحيما ٩٦
دَرَجَـٰتٍۢ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةًۭ وَرَحْمَةًۭ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًۭا رَّحِيمًا ٩٦
دَرَجَٰتٖ
مِّنۡهُ
وَمَغۡفِرَةٗ
وَرَحۡمَةٗۚ
وَكَانَ
ٱللَّهُ
غَفُورٗا
رَّحِيمًا
٩٦
Ni vyeo hivyo vinavyo toka kwake, na maghfira na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Thawabu nyingi hizi ni daraja za juu, katika mabustani ya Pepo, zitokazo kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, walizopewa waja Wake maalumu wenye kupigana katika njia Yake, na msamaha wa madhambi yao na rehema kunjufu ambayo ndani yake wananeemeshwa. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa anayetubia Kwake na kurejea, ni Mwingi wa rehema kwa wenye kumtii, wenye kupigana jihadi katika njia Yake.