Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nur 24:28

24:28
فان لم تجدوا فيها احدا فلا تدخلوها حتى يوذن لكم وان قيل لكم ارجعوا فارجعوا هو ازكى لكم والله بما تعملون عليم ٢٨
فَإِن لَّمْ تَجِدُوا۟ فِيهَآ أَحَدًۭا فَلَا تَدْخُلُوهَا حَتَّىٰ يُؤْذَنَ لَكُمْ ۖ وَإِن قِيلَ لَكُمُ ٱرْجِعُوا۟ فَٱرْجِعُوا۟ ۖ هُوَ أَزْكَىٰ لَكُمْ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌۭ ٢٨
فَإِن
لَّمۡ
تَجِدُواْ
فِيهَآ
أَحَدٗا
فَلَا
تَدۡخُلُوهَا
حَتَّىٰ
يُؤۡذَنَ
لَكُمۡۖ
وَإِن
قِيلَ
لَكُمُ
ٱرۡجِعُواْ
فَٱرۡجِعُواْۖ
هُوَ
أَزۡكَىٰ
لَكُمۡۚ
وَٱللَّهُ
بِمَا
تَعۡمَلُونَ
عَلِيمٞ
٢٨
Na msipo mkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini. Hivi ni usafi zaidi kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na iwapo hamtampata mtu kwenye nyumba za watu wengine, basi msizingie mpaka aweko mwenye kuwaruhusu. Asiporuhusu na akasema, «rudini,» basi rudini, wala msisisitize kutaka kuruhusiwa, kwani kurudi wakati huo ni jambo zuri zaidi kwenu, kwani mwanadamu ana nyakati na hali ambazo hapendi kwenye hali hizo kuonekana na mtu mwingine. Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda ni Mjuzi na Atamlipa kila mtendaji kitendo chake.