Na wanasema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tumet'ii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala hao si wenye kuamini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wanafiki wanasema, «Tumemuamuni Mwenyezi Mungu na yale ambayo amekuja nayo Mtume na tumezitii amri zao.» Kisha vinatoka vikundi kati yao, baada ya hapo, vikayapa mgongo hayo, visiukubali uamuzi wa Mtume. Basi hao hawakuwa ni Waumini.