Msiwadhanie walio kufuru kwamba watashinda katika nchi. Na makaazi yao ni Motoni, na hakika ni maovu kweli marejeo yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Msidhani tena msidhani kwamba wale waliokufuru wanamshinda Mwenyezi Mungu katika ardhi, kwani Yeye ni Muweza wa kuwaangamiza, na marejeo yao, huko Akhera ni Motoni. Na ni mabaya sana marejeo haya na mwisho huu. Maneno haya ni maelekezo kwa ummah wote, ingawa anayeambiwa hapa ni Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.