Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nur 24:59

24:59
واذا بلغ الاطفال منكم الحلم فليستاذنوا كما استاذن الذين من قبلهم كذالك يبين الله لكم اياته والله عليم حكيم ٥٩
وَإِذَا بَلَغَ ٱلْأَطْفَـٰلُ مِنكُمُ ٱلْحُلُمَ فَلْيَسْتَـْٔذِنُوا۟ كَمَا ٱسْتَـْٔذَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌۭ ٥٩
وَإِذَا
بَلَغَ
ٱلۡأَطۡفَٰلُ
مِنكُمُ
ٱلۡحُلُمَ
فَلۡيَسۡتَـٔۡذِنُواْ
كَمَا
ٱسۡتَـٔۡذَنَ
ٱلَّذِينَ
مِن
قَبۡلِهِمۡۚ
كَذَٰلِكَ
يُبَيِّنُ
ٱللَّهُ
لَكُمۡ
ءَايَٰتِهِۦۗ
وَٱللَّهُ
عَلِيمٌ
حَكِيمٞ
٥٩
Na watoto wanapo fikilia umri wa kubaalighi basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyo kubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na pindi watoto wanapofikia miaka ya kubaleghe na kukalifishwa hukumu za kisheria, ni juu yao watake ruhusa wakitaka kuingia nyakati zote kama wanavyotaka ruhusa watu wazima. Na kama Mwenyezi Mungu Anavyowafafanulia adabu za kutaka ruhusa (kuingia majumbani), vilevile Anawafafanulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, aya Zake. Na Mwenyezi Mungu Anayajua sana yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake.