Yeye ndiye anaye kuonyesheni umeme kwa khofu na tamaa, na huyaleta mawingu mazito. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yeye Ndiye Ambaye anawaonesha umeme, nao ni mwangaza unaong’aa kutoka ndani ya mawingu, mkawa mnaogopa msishukiwe na vimondo venye kuchoma kutokana na umeme huo, na pia mkawa mnatazamia mvua inyeshe. Na kwa uweza Wake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, anayleta mawingu yanayobebeshwa maji mengi kwa ajili ya manufaa yenu.