Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ar-Raad 13:14

13:14
له دعوة الحق والذين يدعون من دونه لا يستجيبون لهم بشيء الا كباسط كفيه الى الماء ليبلغ فاه وما هو ببالغه وما دعاء الكافرين الا في ضلال ١٤
لَهُۥ دَعْوَةُ ٱلْحَقِّ ۖ وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَىْءٍ إِلَّا كَبَـٰسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى ٱلْمَآءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَـٰلِغِهِۦ ۚ وَمَا دُعَآءُ ٱلْكَـٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍۢ ١٤
لَهُۥ
دَعۡوَةُ
ٱلۡحَقِّۚ
وَٱلَّذِينَ
يَدۡعُونَ
مِن
دُونِهِۦ
لَا
يَسۡتَجِيبُونَ
لَهُم
بِشَيۡءٍ
إِلَّا
كَبَٰسِطِ
كَفَّيۡهِ
إِلَى
ٱلۡمَآءِ
لِيَبۡلُغَ
فَاهُ
وَمَا
هُوَ
بِبَٰلِغِهِۦۚ
وَمَا
دُعَآءُ
ٱلۡكَٰفِرِينَ
إِلَّا
فِي
ضَلَٰلٖ
١٤
Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanao waomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayafiki. Na maombi ya makafiri hayako ila katika upotovu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ni wa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Peke Yake, ulinganizi wa tawhīd «Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu.» Haabudiwi wala haombwi isipokuwa Yeye. Na waungu ambao wao wanawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawaitiki maombi ya mwenye kuwaomba. Na hali yao pamoja na hao waungu ni kama hali ya mwenye kiu anayenyosha vitanga vyake viwili vya mkono kwenye maji kutoka mbali ili yafike kwenye kinywa chake, yakawa hayafiki. Na maombi ya makafiri kwa hao waungu hayakuwa isipokuwa yako mbali na usawa, kwa kuwa wao wanamshirikisha wengine pamoja na Mwenyezi Mungu.