Na ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashika Swala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya Akhera. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Nao ndio ambao walivumilia udhia na kusimama juu ya utiifu na kujiepusha na uasi kwa kutafuta radhi za Mola wao, walitekeleza Swala kwa namna iliyotimia zaidi, walitekeleza Zaka za lazima za mali yao na matumizi yanayopendekezwa kwa siri na kwa dhahiri na wakawa wanaondoa baya kwa zuri lenye kulifuta. Hao wanaosifika kwa sifa hizi watakuwa na mwisho wenye kusifiwa huko Akhera.