Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ar-Raad 13:25

13:25
والذين ينقضون عهد الله من بعد ميثاقه ويقطعون ما امر الله به ان يوصل ويفسدون في الارض اولايك لهم اللعنة ولهم سوء الدار ٢٥
وَٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوٓءُ ٱلدَّارِ ٢٥
وَٱلَّذِينَ
يَنقُضُونَ
عَهۡدَ
ٱللَّهِ
مِنۢ
بَعۡدِ
مِيثَٰقِهِۦ
وَيَقۡطَعُونَ
مَآ
أَمَرَ
ٱللَّهُ
بِهِۦٓ
أَن
يُوصَلَ
وَيُفۡسِدُونَ
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
أُوْلَٰٓئِكَ
لَهُمُ
ٱللَّعۡنَةُ
وَلَهُمۡ
سُوٓءُ
ٱلدَّارِ
٢٥
Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ama waovu, wamesifiwa kwa sifa kinyume na zile za Waumini. Wao ni wale ambao hawatekelezi ahadi za Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa ibada baada ya kujitukulia ahadi ya mkazo. Na wao ni wale wanaokata kile ambacho Mwenyezi Mungu amewaamrisha kukiunga kama vile kukata zao na mengineyo na wanafanya uharibifu katika ardhi kwa kufanya maasia. Hao waliosifiwa kwa sifa hizi mbaya watakalolipata ni kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu na watakuwa na mambo ambayo ni mabaya kwao ya adhabu kali katika Nyumba ya Akhera.