Na wanasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humwacha kupotea amtakaye, na humwongoa anaye elekea kwake, 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na makafiri wanasema kwa kushindana, «Si ateremshiwe Muhammad miujiza inayoonekena kama miujiza ya Mūsā na 'Īsā. Waambie kwamba Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayemtaka miongoni mwa washindani wasiotaka uongofu na haimfai miujiza na Anawaongoza kwenye dini Yake ya haki anayerejea Kwake na kutaka radhi Zake.