Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ar-Raad 13:37

13:37
وكذالك انزلناه حكما عربيا ولين اتبعت اهواءهم بعد ما جاءك من العلم ما لك من الله من ولي ولا واق ٣٧
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَـٰهُ حُكْمًا عَرَبِيًّۭا ۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعْتَ أَهْوَآءَهُم بَعْدَ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّۢ وَلَا وَاقٍۢ ٣٧
وَكَذَٰلِكَ
أَنزَلۡنَٰهُ
حُكۡمًا
عَرَبِيّٗاۚ
وَلَئِنِ
ٱتَّبَعۡتَ
أَهۡوَآءَهُم
بَعۡدَ مَا
جَآءَكَ
مِنَ
ٱلۡعِلۡمِ
مَا
لَكَ
مِنَ
ٱللَّهِ
مِن
وَلِيّٖ
وَلَا
وَاقٖ
٣٧
Na ndio kama hivi tumeiteremsha Qur'ani kuwa ni hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya kukujia ilimu hii, hutakuwa na rafiki wala mlinzi mbele ya Mwenyezi Mungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kama tulivyowateremshia Mitume Vitabu kwa lugha zao, tulikuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani kwa lugha ya Kiarabu, ili uitumie katika kuhukumu. Na lau ulifuata mapendeleo ya washirikina katika kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, baada ya haki iliyokujia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hutakuwa na msaidizi yoyote mwenye kukuhami na kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu isikufikie.