Na ikiwa tukikuonyesha baadhi ya tuliyo waahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe na juu yetu ni hisabu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tukikuonesha , ewe Mtume, baadhi ya mateso tuliyowaahidi maadui zako ya kuhizika na kuungulika ulimwenguni, basi hayo ni yale tuliyowaharakishia. Na tukikufisha kabla hujaona hayo, basi wajibu wako haukuwa isipokuwa ni kutekeleza ulinganizi, na hesabu na malipo ni juu yetu.