Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ar-Raad 13:42

13:42
وقد مكر الذين من قبلهم فلله المكر جميعا يعلم ما تكسب كل نفس وسيعلم الكفار لمن عقبى الدار ٤٢
وَقَدْ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلِلَّهِ ٱلْمَكْرُ جَمِيعًۭا ۖ يَعْلَمُ مَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍۢ ۗ وَسَيَعْلَمُ ٱلْكُفَّـٰرُ لِمَنْ عُقْبَى ٱلدَّارِ ٤٢
وَقَدۡ
مَكَرَ
ٱلَّذِينَ
مِن
قَبۡلِهِمۡ
فَلِلَّهِ
ٱلۡمَكۡرُ
جَمِيعٗاۖ
يَعۡلَمُ
مَا
تَكۡسِبُ
كُلُّ
نَفۡسٖۗ
وَسَيَعۡلَمُ
ٱلۡكُفَّٰرُ
لِمَنۡ
عُقۡبَى
ٱلدَّارِ
٤٢
Na walipanga walio kuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mipango yote. Yeye anajua inayo chuma kila nafsi. Na makafiri watajua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika wale waliokuwa kabla yao waliwapangia njama Mitume wao, kama vile hawa walivyokufanyia. Basi vitimbi vyote vina Mwenyezi Mungu, Anatangua vitimbi vyao na kuwarudishia wenyewe wapite patupu na wajute. Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu Kwake, Anakijua kile ambacho kila mtu anakichuma, chema au kibaya, na atalipwa kwa hicho. Na watajuwa makafiri, watakapofika kwa Mola wao, ni nanani atakuwa na mwisho mwema baada ya dunia hii. Huo ni wa wafuasi wa Mitume. Katika haya kuna onyo na tishio kwa makafiri.