Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wataambiwa washirikina hawa kwa njia ya kulaumiwa, watakapoingia Motoni, «Basi onjeni adhabu kwa sababu ya kughafilika kwenu na Akhera na kujiingiza kwenu kwenye ladha za dunia, sisi tutawaacha kwenye adhabu leo, na onjeni adhabu ya moto wa Jahanamu isiyomalizika kwa yale mliokuwa mkiyafanya duniani ya kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumuasi.»