Hakika wanao ziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwa kweli, wanaoziamini aya za Qur’ani na kuzifuata kivitendo ni wale ambao wanapowaidhiwa nazo au wanaposomewa, wanamsujudia Mola wao kwa kumnyenyekea na kumtii na wanamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumsifu katika kusujudu kwao, na hali wao hawaoni kiburi wakaacha kumsujudia na kumtakasa na kumuabudu Yeye Peke Yake Asiyekuwa na mshirika.